Mshambuliaji wa klabu ya PSG (Paris St-Germain), Neymar amesema kuwa ataenda mahakamani kupinga mashtaka yaliowasilishwa na klabu yake ya zamani Barcelona.

Neymar alihamia PSG kwa kitita cha £200m kilichovunja rekodi mnamo mwezi Agosti baada kununua kandarasi yake.

Wakili wa Neymar amesema kuwa, ”Neymar atawasilisha ombi lake la kujitetea hivi karibuni”.

Barcelona inataka Yuro milioni 8.5 za marupurupu iliomlipa mchezaji huyo baada ya kuandikisha mkataba mpya wa miaka mitano miezi tisa kabla ya kuahamia PSG.

Aidha, Neymar pia anaonekana kusema kuwa Barcelona inafaa kumlipa fedha kufuatia hatua yake ya kuondoka badala ya inavyodaiwa na timu hiyo.

Licha ya marupurupu anayodaiwa katika kandarasi ya 2016, ni muhimu kusema kuwa mchezaji huyo amewasilisha ombi rasmi la kudai fedha zake katika mahakama.

Barcelona ilitaka kulipwa marupurupu iliomlipa mchezaji huyo baada ya kuandikisha mkataba mpya pamoja na asilimia 10 ya kucheleweshwa kwa malipo hayo, ambapo klabu hiyo inamtaka mchezaji huyo kurudisha fedha hizo kwa kuwa tayari alikuwa ameandikisha kandarasi mpya.

Ratiba Ya ELC Mzunguuko Wa Tatu Hadharani
Hofu Yatanda Kambi Ya Ruvu Shooting