Mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG wapo njia panda kufuatia washambuliaji wao Neymar na Kylian Mbappe kuumia wakiwa katika majukumu ya kuzitumikia timu zao za taifa katika michezo ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa usiku wa kuamkia leo.

Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Neymar, alilazimika kutolewa uwanjani dakika nane baada ya mchezo dhidi ya Cameroon kuanza, kwenye uwanja wa MK nchini England.

Mshabiki waliokua na hamu ya kumuona mshambuliaji huyo, walionyesha kuingiwa na simanzi, kufautia hatua ya kuumia kwake na kutolewa  nje ya uwanja.

Naymer ameumia mguu na bado jopo la madaktari wa timu ya taifa ya Brazil, halijatoa taarifa zozote kuhusu vipimo alivyofanyiwa usiku wa kuamkia leo.

Kwa upande wa mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Mbappe ameumia bega wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uruguay uliochezwa jijini Paris.

Brazil's Neymar down injured against CameroonMshambuliaji Neymar alielala chini akiugulia maumivu wa mguu.

Florian Thauvin alichukua nafasi ya mshambuliaji huyo kinda dakika ya 36, hali ambayo ilidhihirisha Mbappe amepatwa na maumivu makali kwenye bega lake wa mkono wa kulia.

Hata hivyo pamoja na wawili hao kuumia, bado timu zao za taifa zilifanikiwa kupata ushindi bao moja kwa sifuri katika michezo hiyo ya kimataifa ya kirafiki.

Kuumia kwa washambuliaji hao wawili, huenda kukawapa wakati mgumu mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG, hususan kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya makundi, ambao utawakutanisha na majogoo wa jiji Liverpool Novemba 28.

Kylian Mbappe picks up a shoulder injury for France against UruguayMshambuliaji Mbappe akiugulia maumivu wa bega

Mchezo huo wa kundi C utachezwa kwenye uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, na PSG watakua na ulazima wa kusaka ushindi ili kujiweka kwenye mzingira mazuri ya kutinga kwenye hatua ya 16 bora.

PSG wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi C, wakizidiwa alama moja na Liverpool, huku SSC Napoli wakiongoza msimamo wa kundi hilo.

Agizo la Museveni kuipiga Taifa Stars lazua gumzo, ‘acha roho mbaya’
Fiesta Vs Wasafi: Fid Q amjibu Babu Tale, ‘hiyo kitu ilinifunza sana’