Mshambuliaji kutoka nchini Brazil na klabu ya Barcelona, Neymar da Silva Santos Júnior, ataukosa mchezo wa kuwania UEFA Super Cup uliopangwa kuunguruma kesho dhidi ya Sevilla FC huko mjini Tbilisi, nchini Georgia.

Uchunguzi wa kitabibu umeonyesha kwamba, mshambuliaji huyo anasumbuliwa na uvimbe wa shavu na huenda ikamchuku siku 14 ama zaidi ili kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida.

Kitengo cha utabibu huko Camp Nou kimeeleza, mbali na kuukosa mchezo wa UEFA Super Cup pia mshambuliaji huyo huenda atakua nje ya kikosi cha FC Barcelona ambacho kitacheza mchezo wa Supercopa de España dhidi ya Athletic Bilbao mnamo August 14 na 17.

Hata hivyo kuna matarajio makubwa kwa Neymar kucheza mchezo wa ufunguzi wa ligi ya nchini Hispania ambapo FC Barcelona wataanza kupambana na Athletic Bilbao.

Daktari Wa Chelsea Arejesha Majibu
Tetesi Za Usajili Barani Ulaya