Ngamia ni mnyama ambaye anafahamika kwa tabia ya upole, unyenyekevu na utii kwa binadamu na huelezwa kuwa pamoja na kwamba humsaidia binadamu kusafiri hasa jangwani, hugeuka kuwa rafiki yake mkuu.

Lakini katika hali ya kustaajabisha, ngamia mmoja katika wilaya ya Barmer nchini India amemng’ata kichwa na kutafuna mwili wa mmiliki wake aliyemfunga miguu siku nzima na kumsahau juani.

Kwa  mujibu wa wakazi wa eneo ambalo tukio hilo limetokea, ngamia huyo alionekana kukasirishwa na kitendo cha mmiliki wake kumuweka juani akiwa amemfunga miguu siku nzima huku akiwahudumia vizuri wageni aliokuwa nao ndani.

Imeelezwa kuwa mtu huyo alishtuka baadae na kubaini kuwa alikuwa amemtesa mnyama wake lakini alipomfungua, ngamia huyo alimrukia na kumng’ata shingo na kichwa. “Alipoanguka chini alimtafuna sehemu mbalimbali za mwili wake na kumuua,” walieleza mashuhuda.

Mashuhuda hao wameiambia Times India kuwa ngamia huyo aliwahi kumshambulia mmiliki wake siku kadhaa zilizopita baada ya kutoridhishwa na namna alivyokuwa akimtunza.

Chanzo: Dailymail.

Ali Kiba azivimbia tuzo, asema ni biashara tu
Video: Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekouture kuanza kutoa huduma kwa watoto njiti

Comments

comments