Jeshi la Polisi mkoani Mara limefanikiwa kumkamata Ngariba Marry Onyango (50) maarufu kwa jina la Mgesi Mwita mkazi wa kitongoji cha Nyahende wilayani Serengeti anayedaiwa kuwakeketa watoto 10 akishirikiana na wazazi wao.

Kamanda wa Polisi mkoni humo, Daniel Shilla amesema mtuhumiwa alikamatwa na Polisi kitengo cha Upelelezi Juni 12 mwaka huu eneo la sirari wilayani Tarime.

”Baada ya kufanya matukio hayo ya kukeketa wasichana alijua polisi wanamtafuta, aliamua kikimbilia nchini Kenya lakini aliendelea kutafutwa na kufanikiwa kukamatw, baada ya kuhojiwa atafikishwa mahakamani ingawa kwa sasa kesi tatu zipo mahakamani amabzo zinamuhusu yeye na baadhi ya wazazi amabo tayari walikamatwa kuhusiana na kitendo hicho” amesema Kamanda shilla

Hata hivyo Kamanda Shilla ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa kuwaripoti katika vyombo vya sheria wale wote wanaojihusisha na vitendo vya ukeketaji pamoja na mila zisizofaa katika jamii ili wachukuliwe hatua.

Naye Mkurugenzi wa shirika la la Hope Fore Girls and women Tanzania linalojishughulisha na kutoa hifadhi ka wasichana wanaokimbia kukeketwa na ndoa za utotoni Rhobi Samweli, amsema amepoka kwa furaha taarifa kukamatwa kwa mama huyo.

Serikali yapiga marufuku Mgonjwa kudaiwa damu kabla ya huduma
Magufuli aalikwa mazishi ya Nkurunziza, Ndumbaro akisaini kitabu cha maombolezo