Uongozi wa Yanga umethibitisha kumsajili mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Mrisho Ngasa ‘Anko’ ambaye alikuwa anachezea Ndanda FC katika msimu uliomalizika hivi karibuni.

Ngasa anarejea Yanga baada ya kumaliza mkataba na Ndanda ya Mtwara.

Muda mfupi kabla dili halijakamilika Ngasa alisema: “Najisikia furaha sana kwa sababu kila ninapokwenda huwa nakumbuka kwamba kuna mchango ambao ninao kwao na wao wanajua.”

Mwenyekiti wa usajili wa klabu hiyo Hussein Nyika amezungumzia kurejea kwa Ngasa ndani ya Yanga.

“Mashabiki wa Yanga wanampenda sana Ngasa na bahati nzuri hapa ni kwake kwa sababu ana mapenzi na anaonesha wazi kwamba anaipenda Yanga, hajifichi.”

“Msimu huu umekuwa mzuri sana kwa Ngasa ameisaidia sana Ndanda kutoshuka daraja.”

Aidha Mrisho Khalfan Ngassa aliwahi kuichezea Yanga kwa miaka kadhaa kabla ya kuamua kwenda Free State ya Afrika Kusini, Fanja FC ya Oman, Mbeya City ya Mbeya na baadae kujiunga na Ndanda FC kabla ya leo hii kutangazwa kurudi Yanga.

Zitto, Mbowe waungana kulichukua jimbo la Bilago
Sakata la matibabu ya Wabunge lamuibua Msekwa

Comments

comments