Diwani wa Kata ya Masama Rundugai jimbo la Hai kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Elibariki Lukasi Mbise amejiuzulu nafasi yake kwa madai kuwa hakuna demokrasia ndani ya chama hicho.

“Kwa hiari yangu mimi mwenyewe, nimeamua kujiuzulu nafasi ya udiwani na nafasi zote ndani ya chama bila kushawishiwa,”amesema Mbise

Aidha, amesema kuwa sababu kubwa ya kuachana na chama hicho ni kukosekana kwa demokrasia ndani ya chama hicho ambayo inaweza kuisaidia jamii katika kutatua matatizo yanayoikabiri.

Ametaja sababu nyingine ya kukihama chama hicho kuwa sera ya Chadema ya kupinga juhudi zote za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo, Mbise ameongeza kuwa ameamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuunga mkono juhudi za kuleta maendeleo zinazofanywa na Rais Dkt. Magufuli.

 

Basi la Kidia One lateketea kwa moto
Video: Mtoto wa Majuto akanusha mama yake kutimuliwa 'ameenda matembezi Dar es salaam'