Mbunge wa viti maalumu (CCM), Jackline Ngaonyani jana alichafua hali ya hewa bungeni mara baada ya kuwatuhumu wapinzani kutafuna rambirambi zilizotolewa katika msiba wa aliyekuwa mbunge mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesambulo.

Aliyasema hayo wakati akichangia katika mjadala wa bajeti ya mwaka 2017/18 baada ya kuzungumzia hoja zake, Ngonyani alitoa salamu za pole zilizotolewa katika msiba wa muasisi wa Chadema.

“Nashukuru sana mwenyekiti, naunga mkono hoja lakini nawaomba wapinzani waache kula rambirambi za msiba wa Ndesamburo maana ni aibu kubwa,”alisema Ngonyani.

Aidha, kauli hiyo iliwafanya wapinzani wacharuke na kumtaka afute maneno hayo ambayo walisema ni ya uchochezi, ambapo mbunge wa Chadema Cecilia Pareso alimvaa na kumuomba afute kauli yake au athibitishe kwa kile alichokisema.

Hata hivyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge kutoa muongozo, Ngonyani alikubali kufuta kauli yake kwa kuwa yalikuwa yanahusu masuala ya msiba.

 

Nchemba aomba radhi bungeni kuhusu walemavu
Himid Mao Mchezaji Bora 2016/17