Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) imepangwa kucheza na DR Congo kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba.

Mchezo wa kwanza utachezwa Tanzania kati ya Machi 30,31 na April 1,2018 na ule wa marudiano utachezwa Congo kati ya Machi 20,21 na 22.

Mshindi katika mchezo huo atacheza na Mali katika raundi ya pili itakayochezwa kati ya Mei 11,12 na 13, 2018.

Wakati huo huo timu ya taifa ya wanawake(Twiga Stars) itacheza na Zambia katika mchezo wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake zitakazochezwa Ghana baadaye mwaka huu.

Twiga Stars inatakiwa kucheza mechi zote mbili kati ya April 2 na April 10,2018.

Mchezo huo ni wa raundi ya kwanza.

Yanga kuchezeshwa na waamuzi kutoka Burundi
Mke wa Mugabe kikaangoni sakata la ‘PhD feki’, mwalimu wake akamatwa