Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeendelea kumkalia kooni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kile ilichoeleza kushindwa kulipia deni la shilingi bilioni 1 kama kodi ya pango.

Taarifa za kuaminika zilizopatakana jana katika jingo hilo lililokuwa na biashara za Mbowe zenye Ukumbi wa Club Bilcanas na gazeti la Tanzania Daima zimeeleza kuwa mali zilizoondolewa kwenye jengo hilo zitapigwa mnada kujaribu kufidia deni hilo.

Kwa mujibu wa Mtanzania, magari yalishuhudiwa yakisomba mali mbalimbali ambapo mmoja wa maafisa wa NHC ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema wanachukua mali ambazo zinaweza kupigwa mnada tu.

Kampuni ya udalali ya Foster ndiyo inayodaiwa kupewa jukumu la kuzipiga mnada mali za Mbowe na walikuwa katika eneo hilo.

Hivi karibuni, Mbowe aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter akipinga hatua hiyo ya NHC kwa madai kuwa sio kweli kama wanamdai kiasi hicho bali kulikuwa na mgogoro wa kimkataba wa muda mrefu baina ya Kampuni yake na  shirika hilo.

Mbowe alidai kuwa hatua hiyo imetokana na ushiriki wake katika masuala ya kisiasa, madai yaliyokanushwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu.

Mhasibu Ashtakiwa kwa kumkashfu Rais Magufuli kwenye Whatsapp
Magufuli awataka CUF kuacha ndoto za mchana