Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatarajia kuutoa ajira zipatazo 26,400 kwa watanzania kupitia mradi wa nyumba 5000, sambamba na kukuza mapato ya Serikali kwa ukusanyaji wa kodi kutoka vyanzo mbalimbali.

Meneja Habari na Mahusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguya ameyasema hayo hii leo jijini Dodoma, na kudai kuwa fedha hizo zinatarajia kupatikana kupitia vyanzo mbalimbali, ikiwemo mauzo ya nyumba, ununuzi vifaa vya ujenzi na kodi ya majengo.

Amesema, mpango huo unaounga mkono sera ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuvutia uwekezaji nchini, na unatarajia kuzinduliwa mwezi Septemba 2022 na taarifa zake zitatolewa mapema.

“Tunatarajia kutoa ajira kwa watanzania kupitia mradi wa SHS wa nyumba 5000 pekee unatarajiwa kutoa ajira zipatazo 26,400 (direct 17,600 na indirect 8,800) na Kukuza mapato ya serikali mfano mradi wa SHS 5000 unatarajiwa kutengeneza mapato ya kodi mbalimbali za serikali TZS bilioni 50,” amesema Saguya.

Saguya ameongeza kuwa, “Ukuzaji wa mapato utatokana na (mauzo ya nyumba) bilioni 10 ( ununuzi vifaa vya ujenzi), PAYE TZS 17.8 bilion, Kodi ya majengo TZS milioni 55, corporate Tax kutoka NHC na wajenzi wengine bilioni 77, VAT 60 bilioni.”

Hata hivyo amefafanua kuwa NHC pia imepanga kuanza utekelezaji wa Sera ya Ubia itakayoruhusu Sekta Binafsi kushiriki katika uendelezaji wa maeneo ya Shirika, yenye lengo la kuharakisha uendelezaji wa maeneo yaliyo wazi katikati ya miji kwa kujenga nyumba za vitega uchumi.

Wakulima mbogamboga kupatiwa maeneo ya wazi mijini
Baba na mwanaye wafungwa maisha kwa uhalifu wa chuki