Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF umesitisha huduma katika vituo vya afya vya mikoa tofauti ambavyo vimebainika kutenda kunyume na makubaliano ya mkataba wa huduma.

Katika barua yao iliyoandikwa Juni 25, 2022 NHIF imevitaja vituo hivyo 10 kutoka mikoa ya Mara, Dar es Salaam, Ruvuma, Mbeya na Mwanza.

Barua hiyo inasema kuwa vituo hivyo 10 vya afya vilifanya udanganyifu katika kuwasilisha madai ya wanachama waliohudumiwa hivyo kukiuka mkataba.

Raila na sera ya kuruhusu mitumba
Makala asimama na 'Ashura'