Madaktari wametumia roboti kwa mara ya kwanza kufanya upasuaji wa macho na kurejesha uwezo wa kuona kwa mgonjwa kwa mara ya kwanza duniani.

Kundi la madaktari kutoka hospitali ya John Radclife nchini Uingereza, walitumia roboti huyo kutoa ngozi nyembamba kutoka jicho la mgonjwa.

Mgonjwa kwa jina Bill Beaver mwenye umri wa miaka 70 aliyefanyiwa upasuaji huo sasa anasema anahisi vyema.

Madaktari wana matumaini kuwa mfumo huo utasaidia katika upasuaji unaohitaji umakini zaidi.

Arsene Wenger: Nilikataa Kazi PSG Kwa Sababu Ya Arsenal
Video: Omary Mtanzania anayeimba Taarabu Canada, asimulia mziki huo unavyokubalika Canada