Mabingwa wa kombe la FA, Arsenal watalazimika kuvuka mitaa na kuwafuata wapinzani wao wa kaskazini mwa jijini London Tottenham Hotspurs, kwa ajili ya kupambana kwenye mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kombe la ligi *Capital One Cup*.
Arsenal waliangukia kwa mahasimu wao, baada ya chama cha soka nchini England FA kuendesha zoezi la upangaji wa ratiba ya mzunguuko wa tatu wa michuano hiyo ambayo huchezwa kwa mfumo wa mtoano.
Michezo mingine ya hatua ya tatu ya kombe la ligi ambayo inatarajiwa kuwa na mvuto pamoja na ushindani ni kati ya Aston Villa ambao watakua nyumbani Villa Park dhidi ya mahasimu wao wa mjini Birmingham, Birmingham City huku Crystal Palace wakipangiwa Charlton.
Ipswich Town watalazimika kusafiri hadi mjini Manchester kwenye uwanja wa old Trafford kupambana na Manchester United, huku mabingwa watetezi Chelsea wakipangiwa kupambana na Walsall huko Bescot Stadium,
Klabu ya Carlisle inayoshiriki ligi daraja la pili nchini England, itakuatana na majogoo wa jiji Liverpool kwenye uwanja wa Anfield, baada ya kufanya kazi kubwa ya kuichabanga QPR mabao 2-1 katika mchezo wa mzunguuko wa pili.
Kwa upande wa Manchester City wamepangiwa kukutana na Sunderland ambao watakua nyumbani Stadium of Light.
Michezo mingine ya mzunguuko wa tatu katika michuano ya kombe la ligi nchini England *Capital One Cup*
Middlesbrough v Wolves
Norwich v West Brom
Hull v Swansea
Leicester v West Ham
Fulham v Stoke
Newcastle v Sheffield Weds
Reading v Barnsley or Everton
Preston v Bournemouth
MK Dons v Southampton
Michezo hii ya mzunguuko wa tatu imepangwa kuchezezwa Septemba 22.