Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kuwa kuna haja kubwa ya dereva ya Mbunge wa Singida Mashariki, Adam Bakari kueleza kwanini alipohisi kuwa wanafuatiliwa na watu wasiojulikana siku ya kushambuliwa kwa Lissu hakuchukua hatua ya kulipeleka gari kituo cha polisi.

Ameyasema hayo Jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema maelezo ya dereva huyo yanatia shaka, wanataka awaeleze mambo kadhaa yatakayosaidia uchunguzi wa tukio hilo.

“Kwa hali ya kawaida ni jambo la kushangaza risasi zote hizo wanasema 38, hata moja haikumpata dereva huyu,” amesema Lugola.

Aidha, kuhusu kuondolewa kwa CCTV Lugola amesema kuwa huo ni upotoshwaji mkubwa ambao unalenga kuwadanganya wananchi na kuwataka waichukie serikali yao na Rais Dkt. John Magufuli na yeye kama waziri wa mambo ya ndani hawezi kukubaliana na hilo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wao ndio walikuwepo katika tukio hivyo wanapaswa kuelezea mazingira halisi ya tukio la waliompiga risasi kama walikuwa wanawake au wanaume wanene au wembamba, warefu au wafupi.

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la anga ashtakiwa kwa ufisadi
Wananchi Makambako waishukia Halmashauri kuhusu fidia