Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Gibson Meiseyeki amekosoa madai ya aliyekuwa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul kuwa miongoni mwa sababu zilizopelekea kiongozi huyo kujiuzulu ni kuwepo kwa michango mingi ndani ya chama hicho.

Moja ya sababu ambayo Pauline Gekul aliitaja wakati akijiuzulu nafasi yake ndani ya CHADEMA hivi karibuni ni kutozwa michango mingi kwa wabunge licha ya chama hicho kupokea ruzuku ya milioni 300 kwa mwezi.

“Kwa mwanachama wa chama chochote kuchangia ni lazima, ni kitu tunakipenda, mbunge kuchanga milioni 2 ni hela ngapi lakini kiukweli hakuna mbunge anayechanga milioni 2, ila kuna gharama kidogo ambazo hata wanaotumia kwenye mitandao wanazitoa.”amesema Meiseyeki

Hata hivyo, amesema kuwa michango hiyo iko kimahesabu hakuna mtu anayeonewa, na haiwezi kuwa ajenda ya mtu kuhama chama bali ni umasikini wa fikra.

Canada yaruhusu matumizi ya bangi kwa tiba
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 17, 2018