Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Julius Kalanga amejibu tuhuma za chama hicho kuhusu madeni anayodaiwa.

Kalanga ambaye alijiuzulu nafasi ya ubunge kupitia Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kuwa ni kweli anadaiwa na baadhi ya taasisi kulingana na shughuli zake anazofanya za kilimo, ufugaji na biashara.

“Ni kawaida kwa mtu yeyote kudaiwa, na ni kweli nadaiwa ila Chadema haiwahusu, wanachokifanya ni siasa za maji taka kutaka kunichafua,”amesema Kalanga

Aidha, amesema kuwa aliamua kuchukua uamuzi wa kujiuzulu na kujiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuona chama hicho kimekosa muelekeo.

Hata hivyo, siku za hivi karibuni lilijitokeza kundi la baadhi ya wanachama wa CCM ambao waliandamana ndani ya jimbo hilo kumpinga mbunge huyo baada ya kusikia tetesi kwamba ameshapitishwa kugombea nafasi hiyo ya ubunge ndani ya chama hicho.

JUKATA Yataka wabunge watungiwe sheria
AFA washindwa kuvunja mkataba wa Pep Guardiola

Comments

comments