Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza shilingi milioni 308 zilizotengwa kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, zitumike kuboresha miundombinu ya barabara Jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wakati akizindua kituo cha Polisi kinachohamishika katika hafla iliyofanyika eneo la Kisasa, Jijini Dodoma na kusema kuwa Rais Magufuli ametoa agizo hilo ili fedha hizo ziende kukarabati miundombinu ya barabara pamoja na taa za kuongezea magari katika barabara ya kisasa.

Amesema kuwa fedha hizo zitatumika pia kukarabati taa za barabarani kwenye barabara mpya ya Emmaus-African Dream yenye urefu wa kilomita 1.4, ambayo kwa sasa inajengwa kwa kiwango cha lami.

Kutokana na msongamano uliopo ambao unaweza kusababisha ajali. Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Magufuli ameamua fedha zote zilizoandaliwa kwa ajili ya maadhimisho hayo zitumike kuboresha barabara. pia ameawataka Watanzania wote waadhimishe siku hiyo ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kufanya usafi katika maeneo yaliyo jirani na makazi yao pamoja na yale ambayo wamezikwa mashujaa ikiwa ni njia ya kuwaenzi,”amesema Majaliwa

Aidha, kufuatia uamuzi huo, Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa waratibu zoezi hilo kwenye maeneo yao yote hapa nchini.

Vile vile, katika hatua nyingine, Majaliwa ameliagiza Jeshi la Polisi lianze kujikita kwenye matumizi ya mifumo ya kiulinzi ya kielektroniki yaani ‘City Surveillance Sytems’ ili limudu kudhibiti hali ya sasa ya uhalifu.

Hata hivyo, kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka Tanzania huadhimisha siku ya mashujaa kama sehemu ya kuwaenzi mashujaa hao ambao waliipigania nchi kwa namna moja ama nyingine.

 

Luis Suarez atangaza vita na Ureno
Diwani wa Chadema azidi kusota rumande