Uamuzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumpokea waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais kumeendelea kuzua hisia nyingi kati ya wanachama wa chama hicho huku uamuzi wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Wilbroad Slaa ukizua sintofahamu.

Sintofahamu hiyo imekuja baada ya ukimya wa Dkt. Slaa ambaye alikuwa anaaminika kuwa ndiye atakayegombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia ngome ya vyama vikuu vya upinzania Ukawa, ambapo licha ya kuonekana katika picha za kikao cha Chadema kilichohudhuriwa na Lowassa, hakuonekana wakati wa utambulisho rasmi wa mgombea huyo.

Sintofahamu hiyo imeongezeka baada ya kuwepo tetesi kuwa Dkt. Slaa aliyekuwa akimtuhumu Lowassa kuwa fisadi na kuliweka jina lake katika orodha ya majina ya mafisadi iliyopewa jina la ‘List of Shame’, amejiondoa katika chama hicho.

Gazeti la Raia Tanzania lililotoka leo limeandika habari kuwa Dk. Slaa ameandika barua ya kujitenga na medani za siasa kwa kuwa hakubaliani na uamuzi wa kumpa Lowassa nafasi hiyo wakati inafahamika kuwa ni mtu aliyetumia fedha nyingi katika mbio za kuomba kuwania urais wa CCM.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu alikanusha tetesi hizo na kueleza kuwa chama hicho kina shunghuli nyingi hivyo  Dkt. Slaa yuko bize na majukumu mengine.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu alisema kuwa chama hicho kiko katika mshikamano imara huku akikiri kuwa kulikuwa na makundi mawili yaliyokuwa yanavutana kuhusu uamuzi wa kumkaribisha Lowassa katika chama hicho lakini mwisho yalikubaliana kwa nia moja.

“Baada ya mjadala wa muda mrefu sana, wajumbe wote tulikuwa kitu kimoja na tukakubaliana kumkaribisha Lowassa,” alisema Profesa Baregu.

Edward Lowassa anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais, leo majira ya saa tano katika makao makuu ya Chadema yaliyoko Kinondoni, Dar es Salaam.

 

 

Mwandosya Athibitisha ‘Kuponda’ Uamuzi Wa Kamati Kuu Ya CCM
Protektion von Informationen gegenwärtig