“Mambo ni hiviii… UFC!” Huu msemo unaoshika kasi mitandaoni unafaa kutumika kwenye tangazo maalum lililotolewa jana kuhusu bingwa wa dunia wa mapigano ya UFC, Canor McGregor kuwa anarejea ulingoni Oktoba 6 mwaka huu kutetea mkanda wake.

Mpiganaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anarejea kwenye ulingo wa mapigano hayo tangu alipompiga Eddie Alvarez, Novemba 2016. Lakini wakati huu anakutana na kisiki kizito zaidi.

Pambano lake la mwisho ni lile la masumbwi kati yake na bingwa wa zamani wa masumbwi duniani, Floyd Maywether, la Agosti mwaka jana lililomuingizia kitita cha $100 milioni. McGregor alishindwa kuhimili masumbwi ya Mayweather katika raundi ya 10, akipigwa KO.

McGregor ambaye amewahi kupoteza mapambano matatu atapambana na mbabe kutoka Urusi, Khabib Nurmagomedov ambaye hajawahi kupoteza pambano akipanda ulingoni mara 26. Wawili hao watawasha moto kwenye UFC 229.

Conor McGregor (kushoto) na Khabib Nurmagomedov

Nurmagomedov anabeba kisasi dhidi ya McGregor ambaye hivi karibuni alishikiliwa na polisi kwa kosa la kushambulia basi lililokuwa limembeba mpiganaji huyo wa Urusi pamoja na wapiganaji wengine.

Hivi karibuni, Nurmagomedov alizungumza baada ya kumaliza pambano lake moja na kueleza kuwa pambano kati yake na McGregor ni pambano rahisi zaidi kwake kuwahi kutokea.

Pambano hili litakaloshuhudiwa Las Vegas, linatajwa kuwa pambano kubwa zaidi kwenye UFC, ambapo McGregor anatarajia kulipwa $25 milioni.

Jaji wa Mahakama ya New York alimpa McGregor adhabu ya kufanya kazi za kijamii pamoja na kupata matibabu ya kudhibiti hasira.

Moise Katumbi apokelewa kwa shangwe katika mji wa Kasumbalesa
Washikiliwa na Polisi kwa tuhuma za utekaji