Uamuzi wa Kamati Kuu ya chama cha ACT- Wazalendo, kujiunga kwenye serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani (SUK), umeanza kupingwa na baadhi ya wafuasi wa chama hicho.

Miongoni mwa waliojitokeza kupinga ushirika huo, ni pamoja na aliyekuwa rais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume ambaye kupitia ukurasa wake wa twitter, amekitaka chama cha ACT kufuatilia historia za mataifa mengine hasa ile ya Zimbabwe ili kusaidia chama hicho kufanya maamuzi sahihi.

“.. mwanzo wa mwisho wa ACT- Wazalendo. Someni historia ya Zimbabwe na Tsvangirai” ameandika Fatma Karume .

 “Maalim (Seif Shariff Hamad) anaaga.Hii ndio miaka yake mitano ya mwisho, nani ataweza kuhamasisha umma mwaka 2025?” amehoji Fatma.

Naye aliyekuwa Mgombea Ubunge wa chama hicho katika jimbo la Nyamagana, Adams Chagulani ameeleza kuwa anapinga maamuzi hayo kwa kuwa hayana faida kwa chama na watu wake, hasa Tanzania Bara.

“Sikubaliani na kilichoamuliwa na chama changu cha ACT- Wazalendo. Uharamu wa nyama ya nguruwe hauondoki kwa kuweka vitunguu swaumu over,” ameandika Chagulani.

Maoni haya yamekuja baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu kusema  chama chake kimeamua kuingia kwenye serikali, kushiriki baraza la wawakilishi na kuingia Bungeni.

'Mo' atoa somo zito Simba SC
Mama ajifungua kuku Kigoma