Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (NHIF), umewataka watoa huduma za afya kuzingatia mikataba waliyoingia na kusisistiza kuwa huduma ya dawa ina dawa nyingi za kuwawezesha watanzania kupata matibabu na hakuna dawa iliyoondelewa .

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mkuu wa NHIF ,Bernard Konga alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kuondolewa kwa baadhi ya dawa zinazotolewa na mfuko huo.

Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao zinadai mfuko huo umeondoa dawa zaidi ya 100 katika huduma zinazotolewa kwa wanachama .

“Hatujatoa dawa na kitita chetu cha huduma za dawa kina dawa zinazotosheleza na kumuwezesha mtanzania kupata matibabu vizuri bila kikwazo chochote,”amesema Konga .

Amesema kuwa mfuko ulifanya marekebisho makubwa sana katika huduma zake ikiwemo eneo la dawa mwaka 2016 na kuweka kitita chenye huduma zaidi ya 11 ikiwamo huduma ya dawa ,na watoa huduma wanatakiwa kuzingatia mikataba walioyoingia ya namna ya kuwahudumia wananchama wake.

Sudan: Mafuriko yapelekea miezi mitatu ya hali ya dharura
Mlipuko waua 16 Bangladesh