Hilo ni moja ya maswali yanayoulizwa na Mashabiki wengi wa muziki wa dansi nchini kufuatia ukimya wa muda mrefu wa msanii huyo mahiri wa muziki wa dansi Tanzania tangu alipitoa wimbo wake wa kwanza muda mfupi baada ya kutoka jela.

Dar24 Media imefanikiwa kumpata Papii Kocha na kufanya naye mahojiano maalumu ambapo ameweka wazi mambo mengi ambayo yamemfanya kukaa kimya kwa kipindi kirefu licha ya mashabiki wake kudhihirisha kiu ya uhitaji wa msanii huyo kuendelea kuachia kazi mara kwa mara.

“Nimeangalia, unajua pia sasa hivi game ime-change, sasa hivi nina Band yangu ambayo niko na ndugu yangu Kalala Junior, inaitwa Tukuyu  tunajipanga, kwa hiyo wasubiri nyimbo zitatoka, nilikuwa na uwezo wa kutoa nyimbo zangu za pembeni lakini nimeziacha kwanza, ntatoa nyimbo za Band halafu baadae nitarudi kama Papii Kocha, nina nyimbo nyingi zaidi ya mia moja” amesema.

Aidha Papii Kocha amedokeza kuhusu maendeleo ya maisha yake ya nje ya Muziki na shughuli ambazo amejikita nazo, hii ni kufuatia fununu zilizokuwa zikienea Mtaani kuwa pengine msanii huyo baada ya kutoka gerezani maisha yake yamekuwa ni duni na labda ndio chanzo cha kupotea kimuziki na hata kutozungumziwa kwenye vyombo vya habari.

” Tuna jambo letu kubwa sana, tuna Band yenye vifaa Tanzania nzima hakuna, na mimi ndio Mkurugenzi nikishirikiana na ndugu yangu Kalala Junior, tukidhaminiwa na Majinja, tuna mabasi tuna Hospital, sasa hata ukiniambia kuonekana kwenye Media halafu sina hela inakuwa haina maana, kwa sasa mimi ni mkurugenzi naendesha vitu vyangu, niko vizuri” aliongeza.

Papii Kocha ameyasema hayo kwenye mahojiano maalumu na Dar24 Media alipohudhuria kwenye hafla ya Ongea na Mama iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hotel ya Serena jijini Dar ea salaam.

"YE" ndilo jina jipya la Kanye West
Kanye West ni Mwendo wa kuisemesha Dunia Non Stop.