Muigizaji na mchekeshaji hodari kutoka nchini Marekani ambaye pia ni mtangazaji wa televisheni Nicholas Scott Cannon maarufu Nick Cannon ameweka wazi kuhusu wakati mgumu anaoupitia yeye na familia yake baada ya kufiwa na mtoto wao mdogo aliyekuwa na umri wa miezi mitano ‘Zen Cannon’.

Jumanne ya Desemba 7, 2021 Nick aliweka wazi taarifa hizo kupitia kwenye kipindi chake cha Televisheni kwamba mtoto wao ‘Zen Cannon’ amefariki Dunia.

Nick amesema kwamba mtoto wake alifariki Jumapili iliyopita kutokana na aina fulani ya saratani ya ubongo iliyokuwa ikimsumbua.

Huku akiwa mwenye majonzi mazito Nick alisimulia habari hizo za kusikitisha mbele ya watazamaji wake na kufunguka kuhusu kipindi kigumu ambacho yeye na familia yake wanapitia kwa sasa. Zen alikuwa mtoto wa saba kwa Nick aliyempata na mkewe mrembo Alyssa Scott.

Hassan Dilunga: Ni mchezo wa kawaida, sio DABI
Diamond, Ali Kiba, Zuchu na Harmonize Waongoza