Nicki Minaj ameamua kufunguka kuhusu tukio la kushambuliwa kwa viatu na Cardi B, akimuonya rapa huyo wa kike kuwa makini anapochagua watu wa kugombana nao.

Mkali huyo wa ‘Chu-Li’ ametumia Queen Radio kufikisha bila chenga onyo lake kwa Cardi, akiwataka watu wanaompenda kumsaidia kuachana na mpango wake kutaka kupigana na watu.

Cardi alimrushia Nicki Minaj viatu akijaribu kumshambulia kwa kile alichodai kuwa alitoa maneno ya dharau na ya uongo dhidi yake na mtoto wake Kulture, lakini hakufanikiwa kumpata na kuishia kupata nundu usoni kutokana na purukushani. Vurugu hizo zilitokea kwenye hafla ya wiki ya mitindo ya New York.

“Hii ni kuhusu kumpa msaada huyo mwanamke. Huyu mwanamke yuko katika hatua bora zaidi ya muziki wake na anaanza kurusha chupa na viatu!?” Nicki alihoji kwa mshangao.

“Ni nani atakayeenda kuingilia na kumsaidi? Nyie jamaa hamuoneshi kujali hadi mtu atakapokufa! Nyie jamaa hamtaki kumzuia hadi mtu atakapokufa… ndipo mtakapoachana na huu upuuzi. Ukiweka mikono yako kwa baadhi ya watu, utakufa. Mwisho!” Nicki alionya.

Hata hivyo, wakati Nicki akitoa onyo lake, watu wa karibu wa Cardi B wameeleza kuwa rapa huyo wa kike hajutii kumrushia Nicki viatu na kwamba endapo angepata nafasi nyingine angemrushia tena viatu kwakuwa alikuwa analinda heshima ya mwanaye.

Cardi anaonekana kuwa rapa wa kike mwenye hasira na hawezi kujizuia. Tukio hilo lilitokea wiki kadhaa tangu alipomwambia shabiki wa Nicki Minaj kuwa amfuate studio wazichape, tena akimuahidi kuwa ataweka mtoto wake mpendwa chini ili apigane naye.

Tunasubiri kuona kama kutakuwa na ngoma za kurushiana maneno kati ya wawili hao. Lakini Nicki ameshaweka wazi kuwa hatakuwa na muda wa kutoa wimbo wa kumshambulia mtu (diss track), lakini atakuwa anatoa ngoma rasmi kali halafu anawachana wabaya wake humo ndani.

Alphonse Areola amvuruga Thomas Tuchel
DC Jokate, Wema waingilia kati sakata la Miss Tanzania 2018

Comments

comments