Nicki Minaj ametamba kuleta mapinduzi makubwa kwenye muziki wake wa hip hop kwa albam yake ya nne iliyoko jikoni ikiwa ni miaka mitatu tangu atoe ‘The Pinkprint’.

Katika mahojiano na DJ Whoo Kid, Nicki amesema kuwa ana uhakika albam yake itapata baraka za kuwa ‘classic hip hop album’, tamko ambalo limeinua vichwa vya mashabiki wengi kwa kuzingatia kuwa bado kuna cheche za bifu na tambo za nani mkali kati yake na Remmy Martin.

“Hicho ndicho kinachofuata kutoka kwenye kapu langu la orodha,” alisema Nicki. “Kuachia albam yangu ya nne na kuhakikisha kuwa inapata baraka za kupokewa kama ‘classic hip hop album’ ambayo watu hawataisahau kamwe,” aliongeza.

Ingawa hakusema lini mzigo huo utaingia sokoni rasmi, alisema ana amini itakuwa kazi yake bora zaidi kuwahi kufanyika na kwamba anachopenda ni kuona jinsi ambavyo mashabiki wake wanaizungumzia kazi hiyo.

Katika hatua nyingine, Nicki alizungumzia tukio la kundi la Young Money kupanda jukwaani kwa pamoja kwenye tuzo za Billboard Charts kumsindikiza Drake aliyeshinda tuzo 13 kwa usiku mmoja.

Nicki alidai kuwa licha ya ukubwa wa Drake na namna ambavyo Lil Wayne anazidi kuwa nguli wa muziki, bado wako timu moja na wanalishana kama ilivyokuwa awali.

Magazeti ya Tanzania leo Juni 9, 2017
Video: Serikali yafuta ada ya mwaka leseni ya magari, yatoa msamaha wa kodi, riba