Malkia wa muziki wa Hip-hop Marekani Onika Tanya Maraj maarufu kama Nicki Minaj amefunguka kuhusu ujio wa albam yake mpya, akiongea na jarida la ‘The New York Times Magazine’ Nick Minaj amedai kwamba albam yake mpya utahusisha maisha yake yote.

”Albamu hii ni kila kitu katika maisha yangu inakuja na stori kamili kuhusu mimi kuwa mkeli na furaha yangu, ni kama kusherekea yote nilopitia” alisema Nicki Minaj akimwambia Roxanne Gay mwadishi aliyemuhoji.

Nicki Minaj aliongeza kuwa katika albam yake iliyopita ya Pink Print ilikuwa kama kitabu na alifunga ukurusa wa baadhi ya mambo lakini hakujua kama ana furaha au huzuni kufungua ukurasa mpya na sasa albam mpya itaeleza maisha yake ya sasa kwa undani.

Album hiyo ambayo bado haijatajwa siku ambayo itaachiliwa rasmi, aliwataka mashabiki zake wafahamu kwamba kila kitu ambacho kimemzunguka kwenye maisha kimewekwa kwenye Album yake.

Wengi wamekuwa wakifikiri kuwa ujio wa wanamuziki wa kike wapya wa Hip-Hop kama Remy Ma na Cardi utamaliza utawala wa Nick Minaj kama malkia wa muziki wa Hiphop kwa wanawake lakini uwezo alionao Nicki huenda akaja kuwafunika na albam mpya.

 

Kenya: Odinga atangaza kuahirisha maandamano, '...tutatangaza hatua tutakayochukua'
Video: Hali ya Lissu inaendelea kuimarika- Mbowe