Imekuwa muda mrefu tangu mkali wa Hip hop kutoka Marekani, Nicki Minaj alipotoa albam ya ‘The Pinkprint’ iliyotoka mwaka 2014 na sasa Malkia huyo mzaliwa wa visiwa vya ‘Trinidad and Tobago’ ametangaza jina na tarehe rasmi atakayoachia albam yake mpya.

Akifanya mahojiano wakati wa onyesho la fasheni la ‘Met Gala’ lililofanyika mjini New York siku ya jumatatu Nicki Minaj alisema anajiskia furaha kwani ni muda wakuieleza Dunia ujio wa albam yake mpya inayoitwa ‘Queen’ itakayotoka tarehe 15 mwezi Juni mwaka huu.

”Bila shaka, nimevaa kama Malkia na hii ni kila wakati”, alisema Nicki alipoulizwa kama ana muonekano wa Malkia. Tayari ngoma mbili zitakazo kuwa kwenye albam hiyo zimetoka mpaka sasa ambazo ni ‘Chun-Li’ pamoja na  ‘Barbie Tingz’ na sasa mashabiki wanasubiri ujio wa albam hiyo.

 

Tazama haapa chini Nicki Minaj akitangaza ujio wa albam yake mpya;

 

Walimu wawili watiwa mbaroni kwa kumchoma moto mwanafunzi
Harmonize ‘kulizwa’ na Mwarabu Fighter ilivyonikumbusha ya Jay Z, Bey

Comments

comments