Nicki Minaj ameripotiwa kuachana na timu ya menejimenti yake aliyokuwa nayo kwa muda mrefu zaidi wa kazi yake ya sanaa ya muziki.

Chanzo cha karibu na rapa huyo wa kike kimeuambia mtandao wa Variety kuwa rapa huyo ameachana rasmi na Gee Roberson na Cortez Bryant pamoja na menejimenti ya Blueprint/Maverick.

Sababu rasmi za hatua hiyo bado hazijafahamika lakini inadaiwa kuwa kuna uhusiano na namna ambavyo msanii huyo amekuwa akishindwa kukamilisha baadhi ya miradi yake mikubwa anayowaahidi mashabiki.

Agosti mwaka jana, Minaj aliachia albam yake ya ‘Queen’ iliyofanya vizuri na kushika nafasi ya 2 kwenye Billboard 200. Alitangaza kuwa atafanya ziara yake ya pamoja na Future, ziara ambayo iliahirishwa na haijafanyika lakini pia hakuna tarehe mpya iliyotajwa. Hivi karibuni, ahadi za kuwepo ziara yake ya Ulaya akiwa na Juice WRLD zimegeuka danadana kwa mashabiki wake.

Ingawa kumekuwa na mgogoro wa kiusimamizi, Nicki Minaj aliendelea kushiriki katika miradi ambayo ni jitihada zake akishirikishwa na wasanii wenzake. Hivi karibuni alishiriki kwenye wimbo mpya wa Chris Brown ‘Wobble Up’; na pia wimbo mpya wa Kanye West ambao unatarajiwa kuwa kwenye albam ijayo ya Yandhi.

Ariana kulipwa mara mbili ya Beyonce kwa kazi moja kwazua gumzo
Mahakama yabariki kuondolewa ukomo wa umri wa kuwania Urais

Comments

comments