Rapper Meek Mill ambaye ni mpenzi wa Nicki Minaj ameweka wazi kuwa angependa kumuona mrembo wake huyo akiwa na ujauzito wake.
Meek Mill amefunguka katika mahojiano aliyofanya na kipindi cha radio cha DJ Whoo Kid alipoulizwa kama ana maono ya kutengeneza familia na Nicki Minaj. Rapper huyo wa MMG alisema kuwa anatamani Nicki angekuwa na ujauzito wake, lakini hadi sasa hana.

Muda mfupi baada ya mahojiano hayo, mashabiki walipost kwenye mitandao ya kijamii ombi la Meek na kumtag rapper huyo wa Young Money. Nicki Minaj ambaye jina lake la kuzaliwa ni Onika Tanya Maraj, alijibu kwa tweets kadhaa kabla hajatoa sharti kuwa hawezi kumzalia mwanaume yeyote mtoto kabla ya kufunga nae ndoa.

“No matter wut he, or anyone else says, Onika Tanya Maraj won’t b pushing anyone1 out her vajayjay, until she’s married. Now check that,” aliandika.

Djokovic Atishia Mazingira Ya Ubingwa Wimbledon Open
Angelina Jolie na Brad Pitt Watajwa kuwa Mastaa Wenye Nguvu Zaidi Hollywood