Rapa wa kike Nicki Minaj ambaye ameyapitia maisha magumu akishuhudia unyanyasaji uliofanywa na baba yake dhidi ya mama yake ameweka wazi hasira zake dhidi ya mashairi ya Kanye West kuhusu wanawake weusi.

Akizungumza na jarida la Marie Claire, Nicki Minaj alisema kuwa hakupenda kabisa mashairi ya Kanye kwenye wimbo wake wa ‘Gold Digger’ wa mwaka 2005.

Alisema kipande cha mashairi ya Kanye kinachowaambia wanawake weusi kuwa pale wanaume zao watakapopata fedha watawatosa na kuhamia kwa wanawake weupe kinaumiza na sio cha kufanyia mzaha.

“Nimechoka kuona wanawake weusi tunavyojisikia kwamba wanaume wetu wakipata utajiri watatutosa na kuhamia kwa wanawake wa rangi nyingine,” alisema Nicki.

Hata hivyo, Nicki alieleza kuwa alichokisema Kanye West kilikuwa na ukweli wake kwa sababu hata yeye baada ya kutajirika hivi sasa anaishi na mwanamke mzungu, yaani Kim Kardashian.

Rapa huyo wa Young Money na mchumba wa Meek Mill aliwasihi wanawake hasa weusi kutoolewa kwa misingi ya utajiri wa mwanaume bali waangalie zaidi utu wao na utayari wao.

Video: Mtoto aliyezaliwa bila mikono ajifunza kula kwa miguu, awavuta wengi
Babu Seya, Papii wafunguka kuhusu barua inayodaiwa wamemuandikia Rais Magufuli