Nicki Minaj na Cardi B ambao wamekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu wakitupiana maneno, wakati huu wameungana kumtetea rapa 21 Savage dhidi ya kejeli za mtangazaji maarufu wa Fox News, Tomi Lahren.

Lahren alichokoza moto baada ya kuandika kupitia akaunti yake ya Twitter, Februari 3 mwaka huu  ujumbe wa kejeli kuhusu sakata la 21 Savage kutimuliwa nchini Marekani na Mamlaka ya Uhamiaji baada ya kubainika kuwa sio raia wa nchi hiyo na anaishi bila kufuata sheria za uhamiaji.

“Nina maafisa moja, mbili, tatu, nne, tano, sita, saba, nane wa ICE (Mamlaka ya Uhamiaji) walioko tayari kukutimua,” tafsiri isiyo rasmi ya tweet ya Lahren.

Cardi B alikuwa wa kwanza kumuwakia Lahren akimtaka asimchokoze, “don’t make me get my leash.”

Jana, Nicki Minaj yeye alikuja na msululu wa mashambulizi dhidi ya mtangazaji huyo ambaye alianza kujipatia umaarufu kwa kuchambua masuala ya siasa.

“Mtazamo wako kwenye utamaduni wetu unaogopefya, niseme kidogo tu. Sipendi kukupa kiki unayoitafuta kwa hamu. Kuwacheka watu kwa sababu tu wanafukuzwa Marekani kama vile babu zako wewe ndio walioigundua Marekani. Hivi wewe ni mzawa wa Marekani?” inasomeka tafsiri isiyo rasmi ya tweet ya Nicki Minaj ambayo iliunganishwa na matusi pia.

Mtangazaji huyo alilazimika kujitetea katika kila mashambulizi aliyopewa na marapa hao wa kike, akiwataka kutokumbatia tabia ya wageni kuishi nchini Marekani bila kufuata sheria na taratibu.

Cardi B amewahi kufanya wimbo na 21 Savage, na ni mmoja kati ya wakali anaowakubali na amefanya naye ngoma inayoitwa ‘Bartier Cardi’. Nicki Minaj pia anamkubali sana rapa huyo na ameshiriki naye kwenye wimbo ‘No Flag’ wa London On Da Track.

21 Savage

ICE wamebaini kuwa 21 Savage ni mzaliwa wa Uingereza aliyehamia Marekani mwaka 2005 na kwamba baada ya kibali chake cha kuishi kufikia ukomo alianza kuishi bila kuwa na kibali hadi mwaka huu.

Daily Maily ya Uingereza wiki hii imetoa nyaraka ikiwa ni pamoja na nakala ya cheti cha kuzaliwa kinachoonesha rapa huyo ni mzawa wa Uingereza.

Serikali Yatoa notisi ya Siku 24 Kuhuisha Machapisho
Ommy Dimpoz afunguka ya moyoni, Jokate & Jux wampa neno

Comments

comments