Onika Tanya Maraj maarufu kama ‘Nicki Minaj’, wiki hii ndiye rapa wa kike aliyewapa ‘umatemate’ mashabiki wa muziki wa rap duniani akiandaa kupakua ngoma mbili mpya kwa mkupuo.

Nicki ameachia kionjo cha wimbo wake mmoja alioupa jina la ‘Barbie Tingz’, kionjo ambacho kimegeuka gumzo kwenye mitandao ya kijamii. Nyimbo zote mbili zitaachiwa rasmi leo.

Rapa huyo anapita kwenye midundo inayofanana na ile ya miaka ya 1980, enzi hizo ‘muziki wa rap ukiitwa muziki wa rap’.

Kwenye ‘Barbie Tingz’, anawashushia tambo na kejeli kwa wale anaodai wanashida kwenye mitandao wakitaka kuiga muonekano wake na muziki wake.

Chuma cha pili anachoachia Nicki leo hii ni ‘Chun-Li’, jina la staa wa kike kwenye filamu ya mapigano ya ‘Street Fighter II’.

Nyimbo hizi zitakuwa kwenye albam ya nne ya Nicki inayosubiriwa kwa hamu tangu alipoachia ‘PinkPrint’ mwaka 2014.

Amshambulia mkewe kwa mapanga kisa kunyimwa unyumba
Video: JPM awapandisha vyeo wanajeshi

Comments

comments