Baada ya tetesi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Nicki Minaj anamahusiano  na mwendesha magari yaendayo kasi, Lewis Hamilton sasa huenda isiwe tetesi tena kwani wawili hao wameonekana wakiwa karibu katika picha zilizosambaa mtandaoni.

Rapper Nicki Minaj mwanamziki maarufu nchini marekani na Lewis Hamilton champion wa magari yaendayo kasi wameposti picha kwenye kurasa zao za mtandao wa Instagram, wakiwa wawili mjini Dubai.

Image result for nicki minaj and lewis

Lewis ambaye amewahi kuchukua ubingwa wa dunia kwa mara ya kwanza akiwa na McLaren 2008, na baadae kuhamia Mercedes ambapo alishinda ubigwa wa dunia mara mbili mwaka 2014 na 2015 kabla ya kushinda ubigwa mwingine mwaka 2017.

Amezaliwa na kukulia Stevenage, Hertfordshire Hamilton alianza kupenda race mara baada ya baba yake kumpeleka kuwa  radio-controlled car alipokuwa na miaka sita na kujiunga na McLaren’s young driver support programme 1998.