Hatimae aliyekua mshambuliaji wa Arsenal Nicklas Bendtner, amerejea nchini England na kusaini mkataba na klabu ya inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Nottingham Forest.

Bendtner mwenye umri wa miaka amerejea nchini humo akitokea nchini Ujerumani ambapo alikua akiichezea klabu ya Wolfsburg inayoshiriki ligi ya Bundesliga.

Mwenyekiti wa klabu ya Nottingham Forest, Fawaz Al-Hasawi amethibitisha kukamilishwa na mpango wa kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo kutoka nchini Denmark kama mchezaji huru.

Fawaz amethibitisha taarifa hizo kwa kuandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

Usajili wa Bendtner huenda ukawa na changamoto kubwa kwake, kufuatia klabu ya Forest kutarajia kupambana na Arsenal katika mchezo wa kombe la ligi (EFL Cup) majuma mawili yajayo.

Alipokua na klabu ya Arsenal, Bendtner alifanikiwa kucheza michezo 171 na kufunga mabao 47, kabla ya kupelekwa kwa mkopo nchini Italia kwa mabingwa wa Sirie A Juventus FC.

Pia aliwahi kutolewa kwa mkopo katika klabu za Birmingham City na Sunderland zote za nchini England.

Mwaka 2014 baada ya mkataba wake na Arsenal kufikia kikomo alitimkia nchini Ujerumani na kujiunga na VfL Wolfsburg.

Serikali inafikiria nini kuhusu deni la taifa?
Video: Serikali kuanza ujenzi nyumba za wakazi wa Magomeni Kota