Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) imebainisha kuwa haitakuwa rahisi kwa mtu yoyote raia wa Tanzania kumiliki simu kama hatakuwa na kitambulisho cha Taifa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIDA, Rose Mdami, ambapo amesema kuwa pamoja na mambo mengine kwa sasa mamlaka hiyo inaendelea na usajili wa wananchi katika mikoa 20 ya Tanzania Bara, huku kwa upande wa Zanzibar zoezi likiwa limekamilika.

Amesema kuwa NIDA inaendelea kusajili Mamlaka za Udhibiti wa mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA) kwa lengo la kusajili wanachama na wanufaika wote wa mifuko hiyo nchini.

“Majaribio ya zoezi hilo yanafanyika katika mikoa sita, kwa Dar es Salaam ni Mliman City, hivyo wananchi wanaokwenda kusajili laini za simu kama hawana vitambulisho vya taifa basi wanashauriwa kwenda kwenye ofisi za NIDA wilaya ili wapate vitambulisho kwa sababu mfumo utakuwa unamtambua mtu kwa alama za vidole.”amesema Mdami.

Akizungumzia gharama za mradi huo Rose amesema mradi hadi kukamilika unategemea kugharimu kiasi cha dola za Marekani 149 milioni, ambazo ni wastani wa sh. 335.3 bilioni.

Aidha, katika awamu hii ambayo inaendelea NIDA inawafuata wananchi katika ngazi ya Kata, vijiji na mitaa, lakini baada ya awamu hiyo kuisha watakaohitaji watatakiwa kwenda katika ofisi za mamlaka hiyo ngazi ya wilaya.

Hata hivyo ameongeza kuwa pamoja na usajili wa wananchi NIDA inaendelea na zoezi la kuwasajili wafanyabiashara na wachimbaji katika mgodi wa Mererani mkoani Arusha.

Video: Jokate atenguliwa uongozi UVCCM, Askofu Shoo asema kanisa halitazibwa mdomo
Magazeti ya Tanzania leo Machi 26, 2018