Operesheni ya pamoja ya vikosi vya Niger na Ufaransa kusini magharibi mwa Niger, imewaua magaidi 120 na kukamata vifaa vya kutengenezea mabomu pamoja na magari.

Wizara ya ulinzi ya Niger imesema hadi Februari 20, magaidi 120 walikuwa wameuawa katika operesheni iliyofanyika kwenye mkoa wa Tillaberi karibu na mpaka wa Mali na Burkina Faso.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, hakuna athari zozote zilizojitokeza miongoni mwa vikosi vya Niger na Ufaransa.

Waziri wa Ulinzi wa Niger, Issoufou Katambe ameipongeza operesheni hiyo ya kupambana na magaidi, Maafisa katika mkoa wa Tillaberi wameimarisha taratibu za kiusalama, wameyafunga masoko na kupiga marufuku usafiri wa pikipiki baada ya mashambulizi ya makundi ya wanamgambo ya mwezi Desemba na Januari, kuwaua wanajeshi 174 wa Niger.

Ufaransa ilisema mwaka huu itaongeza wanajeshi wake nchini humo kwa kupeleka wanajeshi wapya 600 ili kukiongezea nguvu kikosi chake chenye wanajeshi 4,500.

Makala: Kibwetere alivyowaua waumini wake kwa moto, akawapumbaza, akapotea kimiujiza
Halmashauri zatakiwa kutumia vijana kukarabati Shule