Jengo lenye ghorofa nne ikiwa ni pamoja na shule, limeanguka mapema leo jijini Lagos nchini Nigeria na kusababisha vifo vya watu takriban 10.

Kwa mujibu wa maafisa uokoaji, shule hiyo iliyokuwa katika ghorofa ya juu zaidi ilikuwa na wanafunzi 100 wakati huo jengo lilipoanguka.

Kwa mujibu wa BBC, kufuatia zoezi la uokoaji takriban watu 40 walifanikiwa kutolewa wakiwa hai.

Serikali ya Nigeria imeeleza kuwa jengo hilo ni moja kati ya majengo yasiyofaa. Lilianguka majira ya saa nne asubuhi kwa saa za Afrrika Magharibi. Watu wengi walishiriki pamoja na kikosi cha uokoaji kuhakikisha wanawaokoa wapendwa wao.

Imeelezwa kuwa bado kuna makumi ya watoto na watu wengine walionasa kwenye vifusi na juhudi za kuwaokoa zinaendelea.

Jengo hilo lilikuwa kwa ajili ya makazi lakini kwa sababu za kibiashara ilifunguliwa shule na baadhi ya maofisi katika jengo hilo.

Matukio ya kuanguka kwa majengo yameshashuhudiwa mara kadhaa jijini Lagos ambapo mwaka 2014, watu 116 walipoteza maisha baada ya jengo kuanguka. Pia, mwaka 2016 watu 100 walifariki baada ya paa la kanisa moja Kusini mwa nchi hiyo lilipoanguka.

Video: Simulizi ya Mbowe gerezani inaliza, Maalim Seif abakisha saa chache CUF
Profesa Lipumba ashinda uenyekiti CUF kwa kishindo

Comments

comments