Serikali ya Nigeria imechukua hatua ya kutoa tiba kwa wananchi wake juu ya ugonjwa wa homa ya Lassa ambao umesambaa kwa kasi nchini humo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa ripoti ya ugonjwa huo mwaka 2018 na kubaini kuwa watu zaidi ya 1081 wanadhaniwa kuwa ni waathirika wa ugonjwa huo huku watu 90 wakiwa wamefariki dunia kwa homa hiyo tangu Januari 1 hadi Machi 1 mwaka huu.

Taasisi inayohusika na kudhibiti magonjwa Nigeria, (NCDC), imesema Serikali imechukua uamuzi huo wa kugawa tiba ya ugonjwa huo kwa wagonjwa ambao tayari wanamaambukizi ya homa ya Lassa.

Hata hivyo The Gurdian imefanya utafiti na kubaini kuwa tiba ya ugonjwa huo inagharimu Naila 500,000 kumtibia mgonjwa mmoja wa homa hiyo.

Ripoti ya NCDC, imesema kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo tayari umeathiri majimbo 18 nchini humo na kusababisha vifo vya watu 110 na wagonjwa 1,121.

Mkurugenzi Mtendaji wa NCDC, Dr. Chikwe Ihekweazu ameongea na The Gurdian na kusema kuwa

‘’Tunafahamu gharama kubwa itakayotumika na serikali kutoa tiba ya ugonjwa wa homa ya Lassa nchini, hasa katika dawa ya Ribavirin, lakini tunataka kuwahakikishia wananchi wetu kwamba tiba hiyo itatolewa bure kwa kila mgonjwa aliyeripotiwa kuugua homa hiyo ya Lassa kwa mwaka 2018’’.

NCDC imeongezea kuwa serikali imehakikisha kuwa kila mji ulipo nchini Nigeria unapata akiba ya Dawa ya dawa ya  Ribavirin ili kutibu ugonjwa huo pamoja na vifaa muhimu kukabiliana na homa hiyo pindi atakapotokea mgonjwa.

Ihekweazu, amesema tayari ugonjwa huo umekwisa sambaa katika majimbo matatu, jimbo la Edo, Ondo and Ebonyi hivyo atahakikisha wagonjwa wanapata tiba ya haraka na inayostahili kwani tayari wameshapelekewa vifaa maalumu vya kutibia ugonjwa huo.

Homa ya Lassa iligundulika huko Lassa na kuripotiwa katika jimbo la Borno, homa hiyo inasababishwa na virusi vya Lassa.

Dalili za ugonjwa huu huwa ni homa kali, kutapika, maumivu makali ya kifua na koo kuwasha.

Kutokana na uhaba wa chanjo na dawa za kutibia ugonjwa huo kuwa za ghali, wananchi wanashauriwa kuzingatia usafi katika nyumba zao hasa katika uandaaji wa chakula, pia wananchi wanashauri kuacha kufanya nyama ya panya kama chakula.

Hata hivyo imeshauriwa kuwa mtu aliyekwisha athirika na ugonjwa huo inapaswa atengwe ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kwa watu wengine.

 

 

Mmiliki timu ya Paok amtishia refa bastora baada ya bao kukataliwa.
Hizi chokochoko za wapinzani tunazimudu- Kingu

Comments

comments