Kampuni ya Marekani ya Nike, Inc. inayojihusisha na utengenezaji wa viatu imekana kushiriki katika utengenezaji wa viatu tata vya rapa Little Nas X alivyoviita ‘Satan Shoes’ yaani viatu vya shetani, vyenye tone la damu ya binadamu na taswira za kishetani.

‘Pea’ moja ya viatu hivyo aina ya raba inauzwa $1,018 (sawa na Sh. 2,300,000 za Tanzania).

Kupitia tamko lake lililotolewa Jumapili, Machi 28, 2021, Nike wameeleza kuwa hawana uhusiano wowote na hawakushiriki katika kuandaa kiatu hicho kama rapa huyo anavyodai.

“Hatuna uhusiano wowote na Little Nas X au MSCHF (Kampuni iliyoshiriki katika ukamilishaji wa viatu hivyo) kuhusu kiatu chake anachokiita ‘cha shetani’. Nike haikuhusika kubuni, kutengeneza au kusambaza na hatuviungi mkono,” imeeleza Nike kwenye tamko lake lililotolewa na NBC.

Rapa huyo alizua gumzo na utata wikendi iliyopita baada ya kuonesha viatu vyake aina ya raba, vyenye nembo ya Nike aina ya Air Max ’97. Viatu hivyo vina alama ya ‘x/666, wino mwekundu na tone la damu ya binadamu.

Viatu hivyo vimetayarishwa kwa ushirikiano na kampuni ya MSCHF, pia kinaonesha mstari wa Biblia (Luka 10:18), ambao unaeleza kuhusu kumuona Shetani akishushwa chini kama moto wa radi (Yesu akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme wa radi”).

Hata hivyo, rapa Lil Nas X ameonesha kulikana tamko la Nike akieleza kuwa Nike wameamua kusema uongo wakati walihusika katika utengenezaji wa kiatu hicho.

Awali, Kampuni ya MSCHF ilitoa ina ya kiatu cha Nike Air Max 97 ambavyo waliviita ‘Jesus Shoes (viatu vya Yesu), vilivyokuwa na tone la maji ya baraka kwenye sole ya kiatu. Tole hilo lilikuwa la maji yaliyotolewa Mto Jordan. Lakini sasa wamehamia kwa shetani.

Mjumbe NEC: Magufuli alipambania Taifa bila kujali afya yake
Serikali yatangaza tahasusi mpya kidato cha tano