Kampuni ya Nike imetangaza kusitisha mkataba wake na bondia Mfilipino Manny Pacquiao kufuatia kauli yake ya kupinga ndoa za jinsia moja akidai wanaofanya hivyo wanazidiwa akili na wanyama.

Kampuni hiyo ambayo imekuwa ikipinga ubaguzi wa aina yoyote na kutetea watu wanaojihusisha na ndoa za jinsia moja, imeeleza kuwa imechukizwa na kauli za bondia huyo.

“Tumebaini kuwa kauli ya Manny Pacquiao ni ya chuki. Nike inapinga vikali ubaguzi wa aina yoyote na imekuwa na historia ndefu katika kusapoti haki za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja,” Nike wameeleza kwenye tamko lao.

Pacquiao mwenye umri wa miaka 37 amekuwa akifanya kazi na kampuni ya Nike kwa zaidi ya miaka nane.

Akiongea na kipindi kimoja cha Televisheni nchini kwake Manny Pacquiao alisema:

“Ulishawahi kuna wanyama wa jinsia moja wakiwa kwenye uhusiano?,” Pacquiao alihoji. “Kama hakuna uhusiano wa kimapenzi kati ya wanyama wa jinsia moja, basi watu ni wabaya zaidi ya wanyama,” alisema.

Hata hivyo, baadae Bondia huyo aliomba radhi kwa kauli yake lakini aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa haungi mkono ndoa za jinsia moja kwa kuwa ni kinyume na matakwa ya Mungu na maandiko ya Biblia.

Matokeo ya kidato cha nne 2015 yatoka, yako hapa
Ne-Yo kutumbuiza kwenye Mkoa huu Tanzania, Mei 21