Mkuu wa mkoa wa Tabora. Aggrey Mwanri ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani Kaimu Afisa Manunuzi Wilaya ya Sikonge, Silvanus Ndilabika kutokana na kuwepo kwa dalili za ufisadi katika ujenzi vituo viwili vya afya.

Amechukua hatua hiyo leo kwenye ziara yake wilayani humo ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya afya mbalimbali ambapo katika ujenzi wa kituo cha afya cha Kitunda imeonekana kuna ufisadi hivyo kupelekea mradi huo kutokamilika kwa wakati.

”Unaona taratibu za manunuzi hazijafuatwa halafu unaongea kwenye kikao changu kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama unaniambia sikiliza unatoa wapi nguvu hiyo hebu mkamateni huyo”, amesema Mwanri.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amewataka watumishi wa umma mkoani humo kuhakikisha wanabaini kasoro za miradi mapema kabla ya kusubiri yeye ndio akabiani hilo.

Mwanri anafanya ziara yake katika wilaya za mkoa huo kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya.

JPM atumbua mawaziri wawili, Mwita Waitara azidi kung'ara
Mke wa Obama afichua siri alivyowapata watoto wake

Comments

comments