Ni jambo la kawaida kila mtu kutafsiri kitu wa jinsi ambavyo atakuwa ameona au kusikia? na ukiona wasanii wawili wapo pamoja hisia zitaenda mbali kidogo kuhoji kuna nini kinaandaliwa kwa hali ya kawaida unaweza ukadhani kolabo inatengenezwa.

Ilikuwa tofauti pale picha ya Young killer Msodoki akiwa na diamond Plutnumz iliposambaa watu wengi wakajua tayari rapper huyo kutoka mwanza kalamba mkataba WCB kama ilivyokuwa kwa msanii Rich Mavoko.

Young killer ameamua kufunguka na kueleza ukweli wa picha na kwamba watu wanakuwa wepesi kutolea majibu kitu wasichokijua hivyo kwa vile ukiwapa picha wao watajua kuandika habari hivyo hakuna ukweli wowote wa kwamba amesaini mkataba wa lebo ya WCB

”watanzania wanakuambia tuletee picha halafu cha kuandika tutajua hii ilitokana na ile picha niliyopiga na Diamond Platnumz kipindi nilivyoenda ofisini kwake, na kipindi hiko walikuwa wakiendelea na usajili lakini siko kwenye lebo ile ila ikitokea nitaingia kwa kuwa natamani kufika mbali kimuziki” Young Killer aliiambia millard ayo

Aidha msanii huyo amesema Diamond ni msanii ambaye tayari amefika mbali kimuziki kulinganisha na yeye kukutana kwao siyo kwamba mpaka awe chini ya lebo hiyo ila kwasababu ni wasanii inawezekana tukafanya kazi na Diamond amefika mbali kuna vitu anaweza kunisaidia.

”mimi ni solo artist natamani sana kufika mbali na kwa sasa nafasi hiyo sina”

Waziri Mpina Apiga Faini Kampuni Ya Kanji Llji Na Prime Liberty Limited Kwa uchafuzi Wa Mazingira
Komesha Wizi: Sasa unaweza kunasa kilipo kitu chako kwa kutumia simu yako ya mkononi