Rapa Nikki Mbishi ameelezea ujumbe aliopewa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, marehemu Ruge Mutahaba kuhusu muziki wake.

Nikki Mbishi amesema kuwa anakumbuka mara ya mwisho alipokutana na Ruge alimpa sentensi moja yenye maneno machache tata ambayo hadi leo ameshindwa kuyatatua.

“Ruge aliniambia, ‘Nikki Mbishi acha uhuni tufanye biashara’, kwakweli mimi hata leo sijamuelewa moja kwa moja aliongelea uhuni upi,” Nikki aliiambia Pro24.

Nikki ameeleza kuwa marehemu Ruge alikuwa anaukubali uwezo wake na kwamba alikuwa anaona wanaomnyima nafasi kwenye tamasha la Fiesta wanamuangusha.

Alisema hiyo ndiyo sababu iliyomfanya aweke baadhi ya mistari kwenye wimbo wake mpya ‘Priceless’, ambayo anasikika akisema, “Naliamsha dude, hamnipi Fiesta mnamuangusha Ruge.”

“Unajua Ruge alikuwa genius, alikuwa akikusikia kwa mara ya kwanza tu anaweza kujua uwezo wako, na mimi alikuwa ananikubali na alijua kipaji nilichonacho, kwahiyo naamini kutonipa mimi Fiesta hawakuwa wananiangusha mimi, walikuwa wanamuangusha Ruge kwa sababu angependa anione pia kwenye jukwaa,” alisema.

Priceless ni ngoma ya Nikki Mbishi na Wakazi, ambayo imewashika baadhi ya wakali wa rap akiwemo Khaligraph Jones kutoka Kenya, ambaye ameomba ashiriki katika remix yake.

“Khaligraph aliniomba, nimeshamtumia beat kwahiyo anaendelea kufanya, naamini yuko studio anaifanya,” alisema Nikki Mbishi aka Unju.

Lady Jay Dee awachanganya watu, kunani chumbani? ‘uchumba’
Video: Waziri Mpina ateketeza tani 11 za Samaki wenye sumu walioingizwa nchini kutoka China, atoa msimamo mzito

Comments

comments