December 30, 2016 rapa Nikki Mbishi amefunguka kuhusu watu wanaolalamika kuhusu hali ya rapa anayetajwa kuwa mkali wa Freestyle Tanzania, Rashid Makwilo a.k.a Chid Beenz a.k.a Chuma a.k.a Chid wa Ilala na kusema kwamba watu wengi wanaolalamika hawajui ukweli kuhusu Chid.

Nikki Mbishi amesema tatizo la Chid Benz amekuwa hataki kusikia lolote kutoka kwa watu wanaohitaji kumsaidia, na kila akisaidiwa kupelekewa Rehab anatoroka, lakini pia watu wanaompiga picha wengi wao hawajui matatizo ya Chid na wanataka kuonekana tu walikuwa naye.

“Siwezi kupost hata picha yake wala video maana ni fedheha tu ila ukweli ni kwamba nafsi ya CHIDI BENZ haiko tayari kusaidiwa kuacha ngada.  Kwanza kila ukikutana naye anataka aongee yeye tu maneno yake ya lawama na kujiona anaonewa ili hali ana haki sana bila kujali hali aliyonayo kwa sasa.

Kuna waathirika wengi wa madawa ya kulevya hawajawahi hata kujaliwa kwa kupata hata msaada wa kupelekwa REHAB lakini Chid alishikwa mpaka na vitu Airport na yakasawazishwa.  Je,angeshikwa mtu mwingine si ndo ingekuwa n’tolee? He took it for granted, he is ungrateful… Wasaidizi wamechoka pia.  NINI KIFANYIKE na yeye hayuko tayari? – Nikki Mbishi.

Majaliwa achangisha mil.138/- za ujenzi wa shule
Ubize wa wazazi huchangia kuporomoka kwa maadili ya watoto