Busara za msanii Nikki wa pili kupitia mtandao wa kijamii wa Istagram kwenye kurasa wake siku ya leo ameandika maneno ambayo yanatia nguvu kwa aliyemnyonge na kuhisi amesahaulika na wanadamu.

Nikki wa Pili ni moja kati ya wasanii wachache wasomi nchini Tanzania, ambapo amekuwa akitumia elimu yake na kipaji chake kujenga hoja mbalimbali, ameandika hivi kwenye ukurasa wake wa instagram.

”Usife moyo wala usiwe mnyonge eti kwasababu watu hawakusikilizi, hawakupi nafasi, hawatambui uwepo wako, hawakuzingatii, kumbuka Mungu mmiliki wa vyote, muumba wa duniani, akakupa pumzi, akakupa maisha, hakuna zaidi yake sasa kama Mungu alishakuzingatia, anakuzingati, anajua uwepo wako, anakusikiliza, kipi unataka zaidi ya hicho kumbuka mlango unaofunguliwa na binadamu, binadamu mwingine ufunga, ila mlango wake ni wa milele akisha ufungua, Mungu anakuzingatia unyonge wa nini.

Nikki wa Pili ambaye kwa sasa ameanzisha kampeni inayomtaka mtanzania kuwa na mazoea ya kusoma vitabu, katika hamasisha hiyo ameanzisha kipindi chake kinachoruka katika mtandao wa Youtube ambapo anachambua vitabu vilivyaondika na waandishi mbalimbali.

Kwa sasa anachambua kitabu kinachoenda kwa jina la ”Men are From Mars Women are from Venus” kilichoandikwa na mwandishi mashuhuri katika tasnia ya uandishi wa vitabu vya hadithi, John Gray.

 

Ujumbe mzito aliotumiwa bilionea Msuya kabla ya kifo chake
Mtoto wa miaka miwili auawa kinyama

Comments

comments