Baada ya kumalizika kwa mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba katika uwanja wa taifa, Shabiki maarufu wa Yanga, Jimmy amezua gumzo mtandaoni baada ya kutoa chozi hadharani kufuatia kichapo cha bao 1-0 ilichokipata timu yake.

Jimmy amemwaga chozi mbele ya waandishi wa habari akisema kuwa anahofia zaidi juu ya ahadi ambazo aliziahidi kwa wapinzani wake Simba katika mchezo huo.

Aliahidi kuwa endapo Yanga ikifungwa na Simba, atamuweka rehani mkewe na yeye mwenyewe kuvua nguo Kariakoo, ambapo alikuwa akiwaomba mashabiki wa Simba wamsamehe kwa ahadi zake.

Suala hilo limemuibua Afisa Habari wa Simba, Haji Manara ambaye katika ukurasa wake wa Instagram ameandika, “ninakuombea msamaha ili mkeo anusurike!!. Simba ni watu waungwana na kwa kuwa umeomba radhi tunaamini uliyepinga nae atakusamehe pia, ila ‘next time’ iwe fundisho kwa wafuasi wa Mbuteni msithubutu kutoa ahadi kwa bingwa wa nchi,!”.

Baada ya kutoka uwanjani na kufika nyumbani kwake, hali ya Jimmy haikuwa nzuri kwani alikuwa akilalamika mbele ya wazazi na ndugu zake lakini akishindwa kueleza nini kinamsumbua.

 

Wachimbaji wa madini Njombe wampongeza JPM
Video: Makonda amjibu Tundu Lissu, Simba hii sasa sifa

Comments

comments