Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa onyo kali kwa watu wanaopanga maandamano na kusema atawashughulikia ili wakawasimulie watu waliowatuma.

Ameyasema hayo hii leo wakati akizindua tawi la benki ya CRDB Chato, ambapo amesema kuwa wapo watu ambao wanataka kuona amani ya nchi hii inavurugika jambo ambalo yeye hawezi kukubali kwa kuwa aliapa kulinda Katiba ya nchi.

“Nimeshasema ngoja waandamane wataniona, kama kuna baba zao wanawatuma basi watakwenda kuwasilimulia vizuri, niliapa kwa Katiba kwamba nchi hii lazima iwe ya amani na tunataka tujenge uchumi wa kweli ili Watanzania watajirike na hali ya Watanzania imeanza kwenda vizuri mwanzo ni mgumu lakini nataka niwaambie watanzania tupo kwenye wakati mzuri tuvumiliane ili tufike sehemu Tanzania iwe nchi ya asali,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli ameupongeza uongozi na Bodi ya CRDB, kwa kufungua tawi la benki hiyo wilaya ya Chato mkoa wa Geita.

Young Africans Vs Township Rollers yaingiza milioni 56,245,000
Florida wapitisha muswada wa usalama shuleni