Mtoto wa Kwanza wa Rais wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ametangaza nia yake ya kugombea kiti cha Urais wa nchi hiyo akisema amechoka kusubiri huku akiwasuta Viongozi wakongwe akiwemo baba yake, Yoweri Museveni na mjomba wake, Jenerali Salim Saleh, kwa kuendelea kutawala kizazi kipya.

Afisa huyo wa kijeshi mwenye umri wa miaka 48 na mshauri wa rais katika masuala ya oparesheni maalum ameonesha nia yake na kusubiri zamu yake ya kuiongoza Uganda kwa hamu kubwa akisema wakati umewadia.

Tweet ya Muhoozi Kainerugaba

Amesema, “Waziri Mkuu wa Uingereza ana umri wa miaka 42, Waziri Mkuu wa Finland ana miaka 37. Baadhi yetu wana umri wa miaka 50. Tumechoka kusubiri milele. Tutachukua msimamo! Fidel Castro, SHUJAA wangu, alikua Rais akiwa na miaka 32.”

Sehemu ya hoja za Muhoozi alizozichapisha katika ukurasa wake wa Twitter.

“Ninakaribia kufikia umri wa miaka 49. Kweli sio sawa. Urais wa taifa umekusudiwa kwa vijana. Ni wangapi wanaokubaliana nami kwamba wakati wetu umefika? Inatosha kusema wazee wanaotutawala sasa inatosha kututawala,” amefafanua Muhoozi.

Ramaphosa, Samia wazungumzia Biashara, uwekezaji
Wakimbizi 3000 wa Kongo waomba hifadhi Tanzania