Aliyekuwa diwani wa Kata ya Olsunyai mkoani Arusha, Elirehema Nnko kwa tiketi ya (CHADEMA) ambaye amekihama chama chake na kujiunga CCM amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaangalia watu wa kuwachukua kutoka upinzani.

Ameyasema hayo wakati akihojiwa na moja ya chombo cha habari na kusema kuwa yeye amechukuliwa na CCM kwa kuwa anajiweza na kudai ili uchukuliwe na CCM basi lazima uwe jembe kwani kitu kizuri kinajiuza.

“kamwe Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi na idara zake zote hatutoruhusu mtu atutoe katika agenda ya msingi ya maendeleo ya nchi hii kwa kutengeneza vitu vya kipuuzi tu. Kuna mtu anawataka watanzania waache fursa hizi za elimu, ajira kupitia viwanda vilivyopo nchini eti wakaandamane. Sasa kama kuna wapuuzi wawili watatu mimi nasisitiza tu wajaribu na waone.Inapotokea suala la ulinzi na usalama wa nchi hii, vyombo vyetu vipo imara katika hilo,”amesema Nnko.

 

Vipaza sauti msikitini vyapigwa marufuku
Video: Lissu - Mwili wangu umejaa vyuma, Mwili wa tajiri wa mabasi wakutwa kwenye kiroba